Monday, July 27, 2015

MKUTANO WA UJIRANI MWEMA NCHI YA TANZANIA NA ZAMBIA MIKOA YA MPAKANI (RUKWA NA JIMBO KASAMA KASKAZINI) KUJADILI UDHIBITI WA MAGONJWA AMBUKIZI

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha kulia na Mganga Mkuu wa Jimbo la Kasama Kaskazini Zambia Dkt. Lawrence Phiri wakikabidhiana maazimio ya pamoja ya kuendesha itifaki ya ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili katika kupambana na magonjwa yanayoambukiza maeneo ya mpakani. Anaeshuhudia katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta aliyeongoza Mkutano huo  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya, Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Kalambo Falls Mjini Sumbawanga tarehe 25 Julai 2015.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo na Wageni kutoka jimbo la Kasama Kaskazini (Kasama North Province).

Thursday, July 16, 2015

MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa na kuanza ziara zake Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2015. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (wa nne kulia mbele) na wakimbiza mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2015 baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (wa kwanza mbele) na wakimbiza Mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Kalundi Wilayani humo tarehe 14 Julai 2015. 
Moja ya mtambo wa kisasa wa umwagiliaji katika shamba la umwagiliaji la Ntatumbila Wilayani Nkasi. Mradi huu wa shamba la umwagiliaji na mifugo lina ukubwa wa hekta 1,000 na linamilikiwa na kuendeshwa na wazawa ambapo mpaka kukamilika kwake utagharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 46.
Miongoni mwa wamiliki wa shamba hilo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Juma Khamis Chum wakipiga picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru mara baada ya uzinduzi wa mradi wa umwagiliaji katika shamba hilo la Ntatumbila Wilayani Nkasi.

Saturday, July 11, 2015

MWENGE WA UHURU WAANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Wilaya ya Momba Richard Mbeho kushoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya leo tarehe 11 Julai 2015 tayari kwa kuanza mbio zake za siku nne Mkoani Rukwa. Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni 11. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akishika Mwenge wa Uhuru ulipowasili  Mkoani Rukwa leo tarehe 11 Julai 2015.
 
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkutano Mkoani Rukwa wakiwa wamebeba bendera ya taifa kwa ajili ya kuipeleka na kuipeperusha eneo la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda Mkoa wa Rukwa.
 Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akishika mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili Mkoani Rukwa leo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi mradi wa maji ya mserereko katika kijiji cha Kamnyazia Wilayani Sumbawanga leo katika ziara ya mbio za mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa.
Sehemu ya wananchi wakishuhudia mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa leo.


Friday, July 3, 2015

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA NDUGU ERASMUS RUGARABAMU AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA SIKU SITA YA WALIMU WAKUU NA WARATIBU ELIMU KATA JUU MUONGOZO WA UENDESHAJI SHULE NA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI WA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI RUKWA

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku sita ya Walimu Wakuu Shule za Msingi na Waratibu Elimu Kata juu ya muongozo wa uendeshaji wa shule (School Management Tool Kit) pamoja na usimamizi wa ufundishaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu leo tarehe 03 Julai 2015. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu yanafanyika Mkoani Rukwa katika Chuo cha Ualimu Sumbawanga ambapo jumla ya washirikia 200 kutoka Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga Vijijini wameshiriki kwenye awamu hii ya kwanza ya mafunzo. Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa BRN wenye lengo la kuinua ubora wa elimu nchini.
 Ndugu Nicholaus Moshi ambae ni Mratibu wa Programu ya Mafunzo ya Waalimu Kazini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza katika Semina hiyo. Ndugu Moshi ni mmoja ya wawezeshaji wakuu katika Mafunzo hayo.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
 Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi. Witnes Maeda akitoa nasaha zake katika mafunzo hayo.
Mmoja ya washiriki akitoa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki wote.