Wednesday, June 29, 2016

Mkoa wa Rukwa wapokea Ugeni Kutoka UTUMISHI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa kwanza kulia)akiwakaribisha wageni kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora UTUMISHI  katika Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimkaribisha Katibu Mkuu UTUMISHI Dk. Laurean Ndumbaro ili aweze kuongea na Wakurugenzi, Makatibu Tawala pamoja na wakuu wa Idara za Utumishi. 

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa TEHAMA UTUMISHI, Priscus Kiwango, Mkuu wa Rasilimali watu UTUMISHI Aloyce Msigwa na Mkuu wa mfumo wa Mishahara (LAWSON) UTUMISHI.

Makamu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Aboubakar Kunenge akimwatambulisha Wakurugenzi wa Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa , Wakuu wa Idara za Utumishi katika Halmashauri hizo pamoja na makatibu Tawala wa Wilaya tatu za Mkoa wa Rukwa.

Dk. Hinzi Mastai akitoa malalmiko yake juu ya stahiki zake za kuhamishwa bila ya malipo

Baadhi ya Watumishi waliohudhuria kwenye kikao cha Watumishi wa Umma na Uongozi kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mwalimu Simon Ndungire akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wa UTUMISHI juu ya tatizo la kucheleweshewa kwa malipo ya Likizo na kupandishwa cheo.

Baadhi ya Watumishi waliohudhuria kwenye kikao cha Watumishi wa Umma na Uongozi kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Tuesday, June 28, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa atembelea Mradi wa Barabara ya Mbeya - Kantalamba mjini Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbeya – Kantalamba katika ziara yake ya kuangalia miradi mbalimbali inayofanya na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.

Barabara hiyo ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 1 ni miongoni mwa barabara ambazo zimo katika miradi inyotekelezwa kwa fedha za mfuko wa barabara nchini kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akifafanua umuhimu wa ujenzi wa barabara kuambatana na kukua kwa mji
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga (aliyenyoosha kidole) akifafanua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbeya - Kantalamba mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisaini katika daftari la wageni kwenye eneo la Mradi wa barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa ujenzi wa Barabara ya Mbeya - Kantalamba mjini Sumbawanga alipotembelea katika mradi huo.
Mradi huo wenye gharama ya shilingi Milioni 362.1 ulianza kutekelezwa tarehe 2, Juni, 2016 na kutazamiwa kumalizika tarehe 2, Desemba 2016 na Mkandarasi SUMRY Enterprises Ltd kutoka hapa Mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa aweka jiwe la Msingi Shule ya Sekondari Mhama

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amezindua mradi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari Mhama iliiyopo katika kata ya Malangali, Wilayani Sumbawanga wakati alipofanya Ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.


Mradi huo wa madarasa unagharamiwa na Mpango wa Maendeleo ya Elimu Sekondari (MMES) awamu ya pili kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo mpaka sasa mradi umepokea shilingi Milioni 72 na unatarajiwa kuisha tarehe 30, June, 2016.

Jiwe la Msingi 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa pongezi kwa Mkandarasi wa madarasa mawili aliyoweka jiwe la Msingi

Mtoto wa kidato cha kwanza wa shule ya Mhama Samuel Mbilinyi akisoma kwa nguvu jiwe la Msingi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa mawili matatu mbele ya wananfunzi wa Shule ya Sekondari Mhama mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen na timu aliyoongozana nayo wakiondoka katika shule ya sekondari mhama.

Mkuu wa Mkoa aifundisha SIDO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen ametaka shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kuangalia mahitaji ya wananchi wengi kwa wakati huo ndipo waweze kutengeneza bidhaa zao kulingana na mahitaji hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen akiangalia ngozi inayotengenezwa na wajasiriamali wa SIDO na kutengeneza viatu.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutarahisisha kupata soko ndani ya Mkoa, Tanzania na hata nje ya nchi. “angalieni wananchi wanataka nini kwa kufanya utafiti ndipo mzalishe wanachohitaji ili kupata soko la bidhaa zenu,” alisema hayo alipotembelea shirika hilo ili kutathmini mipango yeke ya kimaendeleo katika Mkoa wa Rukwa.

Ofisi ya SIDO Mkoa wa Rukwa ilifunguliwa mwaka 1975 na mpaka sasa ina wafanyakazi wa kudumu 10 na shirika linatoa huduma mbalimbali ikiwemo mafunzo ya biashara, huduma za ugani pamoja na kuendeleza teknolojia kama kutengeneza sabuni nakadhalika.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.
Pamoja na kutoa huduma hizo SIDO wamekuwa na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kama vile wananchi kuwa na mwamko mdogo katika kushuriki mafunzo mbalimbali yanayotolewa na SIDO na pia wananchi kuchelewa kurudisha mikopo mpaka wapelekwe kwenye vyombo vya sheria lakini pia mifuko ya mikopo ni midogo kulingana na wahitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani) na timu aliyoongozana nayo wakitoka katika ofisi za SIDO

Tangu kuanza kwa shirika hilo mafanikio yaliyopatikana nai pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Mtaa, Halmashauri hadi Mkoa lakini pia watoa ombi kwa Halmashauri kutenga maeneo kwaajili ya wajasiriamali na kuwapa nafasi za kuuza samani katika ofisi zao. 

Mkuu wa Mkoa aahidi kuufatilia Uwanja wa ndege wa Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
“Nimetembelea ili kuona juhudi zinazofanyika kwani, watu wengi wanahitaji hii huduma, sababu kukiwa na uwanja wa ndege unaofanya kazi mambo mengi yatafunguka, kuna utalii kIpili na shemu nyingine,”Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisema.

Mkuu wa Mkoa aliweka angalizo kuwa watu waendlee kusubiri kuona nini kitajiri katika Bunge huko Dodoma kuhusiana na hatma ya Uwanja huo na kuongeza kuwa yupo tayari kufunga safari hadi kwa waziri wa wizara husika ili kulitafutia ufumbuzi suala hili.

“Niko Tayari kwenda jwa waziri wa Ujenzi ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,” Mkuu wa Mkoa alisisitiza.

Mkuu wa Mkoa pia alitoa agizo kwa wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuweka vibao na alama zinazoonyesha kuwa ni Marufuku watu waendao kwa miguu na baiskeli kupita kwenye uwanja huo lakini pia hata wale wanaotumia vyombo vya moto kama vile Pikipiki, Bodaboda na magari.

“Sheria Zifuatwe na mabango yawekwe ili watu wasitumie uwanja kama njia ya kwenda kwa miguu” Mkuu wa Mkoa aliagiza.

Kiwanja kipo daraja la 3c chenye miundombinu inayoruhusu kutua na kuruka kwa ndege zenye uzito usiozidi tani 20 barabara ya kuruka na kutua kwa ndege “Runway” katika kiwanja ni ya changaraw yenye urefu wa mts 1600 na upana wa mts 30 chenye kuhudumia ndege za abiria, ndege za kukodi “charter flights”pamoja na ndege za serikali na muda mwingine huhudumia jamii.

Kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Rukwa safari za ndege zimetoka 57 kwa mwaka 2002 hadi kufikia safari 260 kwa mwaka 2013 na idadi ya abiria kutoka 122 mwaka 2002 hadi kufikia 1131 mwaka 2013.
Meneja wa Uwanja wa ndege wa Manispaa ya Sumbawanga Sandali Issa Kaisi akisoma taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Hayupo pichani)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na maafisa usalama wa uwanja huo wakati alipotembelea uwanja wa ndege wa Mji wa Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za Uwanja wa ndege wa mji wa Sumbawanga. 


Mkuu wa Mkoa aahidi kutembelea shule zote za Rukwa kuangalia ukamilifu wa madawati

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameahidi kugawana na wafanyakazi wake wa Ofisi ya Mkoa kutembelea Shule zote kuhakiki ukamilifu wa madawati katika Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa.

Ametoa ahadi hiyo alipotembelea katika ofisi za Halamashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kuona maendeleo na juhudi zinazofanywa na Halmashauri hiyo katika kutekeleza agizo la Rais D. John Pombe Magufuli la kutotaka kuona mwanafunzi anakaa chini.

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa Maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu juu ya aina ya madawati yanayofaa kwa wanafunzi

Mkuu wa Mkoa alionyesha wasiwasi juu ya ukamilifu wa Madawati hadi kufikia tarehe 30, Juni 2016 na alisema “Sifikirii kwamba mpaka June kama mnaweza kutimiza agizo la Rais” 

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya shule za Msingi za seriakali 55 na Sekondari 17, zenye upungufu wa madawati 5,142 kwa shule za Sekondari na Msingi huku asilimia 99 ya uhitaji huo ni katika shule za Msingi za Manispaa hiyo.

Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndg Mwashusa akisoma taarifa fupi ya hali ya madawati katika Halmashauri ya Manispaa ya  Sumbawanga.
Mchumi wa Manispaa wa Sumbawanga Saad Mtambule alisema kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha katika kufanikisha hili na Mvua nyingi zilizonyesha mwezi Februari hadi Aprili zilisababisha mbao kutokauka mapema.


Lakini pamoja na Hayo Ng. Mtambule alisema “Pamoja na Changamoto hizo kuna Jitihada kadhaa ambazo tunazifanya ili kukamilisha zoezi ikiwemo kupasua mbao katika msitu uliyopo kwenye baabara ya kwenda Kasanga kwa kibali cha TANROAD na pia kuendelea kupasua mbao katika miti iliyopo mashuleni  na kuwashawishi wadau wa maendeleo kuchangia” 


(Kutoka Kulia) Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu.

Monday, June 27, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aweka Jiwe la msingi Ofisi ya Kata Kizwite.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya kata ya kizwite katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika Ziara aliyoifanya kwenye Kata hiyo alipokuwa akitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Manispaa.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephenakifunua kitambaa kilichoficha jiwe la msingi katika ofisi mpya ya kata ya Kizwite
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
akisema " Napenda kusimamia Haki, lazima wote tusimamie haki, Rushwa sipendi, sipendi kuona mambo yanafanyika halafu hakuna uwazi, hayo sitakubaliana nayo, lazima kila nguvu ya kila mmoja isemwe na penye kasoro msisite kuja kwenye ofisi zetu Mkoani na Wilayani, tusiposimamia haki hakuna maendeleo"
Jiwe la Msingi Katika Ofisi ya Kata ya Kizwite

Kata ya Kizwite ni miongoni mwa kata 19 zinazounda Manispaa ya Sumbawanga, kata hiyo ina jumla ya mitaa 15 na jumla ya Wakazi 17,187 kutokana na sensa yam mwaka 2012, na wakazi hao wanajishughulisha na ufugaji, biashara ndogondogo na ukulima.


Katika kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kata ya kizwite ilipata fedah zake kutoka kwa wananchi, wahisani pamoja na Mkurugenzi wa manispaa na kufanya jumla ya fedha kuwa milioni 8.


Mwanafunzi wa Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Ndua iliyopo kata ya Kizwite Debora, akisoma kwa sauti jiwe la Msingi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akionesha wananchi ilani anayoifuata katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanayokusudiwa kwa faida ya kizazi cha leo na cha kesho katika mkutano wa hadhara alioufanya alipokwenda kuweka jiwe la Msingi katika ofisi ya kata ya Kizwite. kuliani kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe


Ofisi ya ata iliyowekewa jiwe la Msingi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika kata ya Kiwite 

Mkuu wa Mkoa aahidi kuwanunulia Uniform Wanafunzi wa Shule maalum ya msingi


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimpa mkono mwanafunzi asiyeona Salum Shabani wakati alipofanya Ziara katika Shule hiyo maalum kwaajili ya wasioona, wenye uoni hafifu na pia wenye ulemavu wa ngozi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameahidi kuwanunulia uniform mpya wanafunzi watano wa darasa la saba wa Shule maalum ya wasioona Malangali iliyopo mjini Sumbawanga baada ya kufanya Ziara Katika shule hiyo kujua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimpa mkono mwanafunzi asiyeona Daniel wakati alipofanya Ziara katika Shule hiyo maalum kwaajili ya wasioona, wenye uoni hafifu na pia wenye ulemavu wa ngozi.

Mkuu wa Mkoa alichukua maamuzi hayo baada ya kuwaona wanafunzi hao wakiwa katika Uniform ambazo haziridhishi kiusafi ambapo wanafunzi hao wote ni wavulana, ili kuweza kuweka usawa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka aliamua kuwauliza wasichana nawao walijibu kuwa hawana shida kwa wakati huu.

Shule maalum ya wasioona Malangali ilifunguliwa rasmi tarehe 8, Agosti, 1998 na Rais wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa. Shule ilijengwa na wamishionari na kanisa katoliki toka nchini Ujerumani, Chini ya usimamizi wa Padri Lukewell na kusajiliwa 2003.

Lengo kubwa la kujengwa kwa shule hii ilikuwa ni kutengeneza fursa kwa walemavu wasioona na kupata haki ya msingi ya elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine wasio na ulemavu.
Shule ya Msingi Malangali inasajili wanafunzi kutoka nchi nzima na mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu 52 pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi 37 na kufanya Jumla ya wanafunzi 89 na waalimu 11.
Wanafunzi wasichana wa Darasa la Saba katika Shule maalum ya MsingiMalangali walipokuwa Darasani wakati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipokuwa Napita kuwasalimia.

Shule ya Msingi Malangali haina upungufu wa madawati ila kuna changamoto mbalimbali ambazo shule imekuwa ikijitahidi kukabiliana nazo ikiwemo upungufu wa madarasa manne , vifaa muhimu vya kujifunzia na kufundishia kama vile mashine za kuandikia maandishi ya wasioona na karatasi maalum, ukosefu wa bweni la wanawake na upungufu wa nyumba za walimu na watumishi.

Katika kukabiliana na changamoto hizo shule imefanya jitihada za kuweza kujikwamua ambapo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeshaainisha miradi miwili yaani ujenzi wa madarasa mawili pamoja na uzio kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, shule imekamilisha mazungumzo na wahisani juu ya ununuzi wa gari mpyalenye thamani ya shilingi milioni 22. Na pia mkuu was hue amefanya mazungumzo na wahisani kutoka Ujerumani na wamekubali kuipatia shule Kompyuta 31, 20 ni Desktop na 11 Laptop.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Nestory Mpendakazi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen namna Printa ya karatasi za nukta Nundu inavyofanya kazi.
Pamoja na jitihada hizo shule imeomba kupewa silaha za moto ili kujilinda kulingana na hali halisi ya mazingira ya shule kwa usalama wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mali za shule.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akipokea maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule maalum ya msingi Malangali katika Bweni la muda la wasichana.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akipokea maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule maalum ya msingi Malangali katika Bweni la  wavulana
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (alieshika kitabu) akiulizia aina ya vitabu ambavyo wanavitumia kila siku katika masomo yao wanafunzi hao wasioona na wenye uoni hafifu .

Sunday, June 26, 2016

Wajue Wakuu wa Wilaya walioteuliwa na Rais Dk John Pombe Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
 1. Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo
 2. Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti
 3. Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka
 4. Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo
 5. Monduli         -           Idd Hassan Kimanta
 6. Karatu                        -           Therezia Jonathan Mahongo


DAR ES SALAAM
 1. Kinondoni     -           Ally Hapi
 2. Ilala                -           Sophia Mjema
 3. Temeke         -           Felix Jackson Lyaviva
 4. Kigamboni     -           Hashim Shaibu Mgandilwa
 5. Ubungo          -           Hamphrey Polepole

DODOMA
 1. Chamwino     -           Vumilia Justine Nyamoga
 2. Dodoma        -           Christina Solomon Mndeme
 3. Chemba         -           Simon Ezekiel Odunga
 4. Kondoa          -           Sezeria Veneranda Makutta
 5. Bahi                -           Elizabeth Simon
 6. Mpwapwa      -           Jabir Mussa Shekimweli
 7. Kongwa          -           John Ernest Palingo

GEITA
 1. Bukombe      -           Josephat Maganga
 2. Mbogwe         -           Matha John Mkupasi
 3. Nyang'wale     -           Hamim Buzohera Gwiyama
 4. Geita               -           Herman C. Kipufi
 5. Chato             -           Shaaban Athuman Ntarambe

IRINGA
 1. Mufindi          -           Jamhuri David William
 2. Kilolo             -           Asia Juma Abdallah
 3. Iringa              -           Richard Kasesela

KAGERA
 1. Biharamulo   -           Saada Abraham Mallunde
 2. Karagwe         -           Geofrey Muheluka Ayoub
 3. Muleba          -           Richard Henry Ruyango
 4. Kyerwa           -           Col. Shaban Ilangu Lissu
 5. Bukoba          -           Deodatus Lucas Kinawilo
 6. Ngara             -           Lt. Col. Michael M. Mtenjele
 7. Missenyi         -           Lt. Col Denis F. Mwila

KATAVI
 1. Mlele              -           Rachiel Stephano Kasanda
 2. Mpanda         -           Lilian Charles Matinga
 3. Tanganyika    -           Saleh Mbwana Mhando

KIGOMA
 1. Kigoma           -           Samsoni Renard Anga
 2. Kasulu                        -           Col. Martin Elia Mkisi
 3. Kakonko       -           Col. Hosea Malonda Ndagala
 4. Uvinza                        -           Mwanamvua Hoza Mlindoko
 5. Buhigwe         -           Col. Elisha Marco Gagisti
 6. Kibondo        -           Luis Peter Bura

KILIMANJARO
 1. Siha                -           Onesmo Buswelu
 2. Moshi             -           Kippi Warioba
 3. Mwanga         -           Aaron Yeseya Mmbago
 4. Rombo           -           Fatma Hassan Toufiq
 5. Hai                 -           Gelasius Byakanwa
 6. Same              -           Rosemary Senyamule Sitaki

LINDI
 1. Nachingwea   -           Rukia Akhibu Muwango
 2. Ruangwa        -           Joseph Joseph Mkirikiti
 3. Liwale             -           Sarah Vicent Chiwamba
 4. Lindi               -           Shaibu Issa Ndemanga
 5. Kilwa              -           Christopher Emil Ngubiagai


MANYARA
 1. Babati             -           Raymond H. Mushi
 2. Mbulu                        -           Chelestion Simba M. Mofungu
 3. Hanang'         -           Sara Msafiri Ally
 4. Kiteto              -           Tumaini Benson Magessa
 5. Simanjiro       -           Zephania Adriano Chaula

MARA
 1. Rorya              -           Simon K. Chacha
 2. Serengeti        -           Emile Yotham Ntakamulenga
 3. Bunda                        -           Lydia Simeon Bupilipili
 4. Butiama         -           Anarose Nyamubi
 5. Tarime           -           Glodious Benard Luoga
 6. Musoma        -           Dkt. Vicent Anney Naano

MBEYA
 1. Chunya          -           Rehema Manase Madusa
 2. Kyela              -           Claudia Undalusyege Kitta
 3. Mbeya                        -   William Ntinika Paul
 4. Rungwe          -           Chalya Julius Nyangidu
 5. Mbarali          -           Reuben Ndiza Mfune

MOROGORO
 1. Gairo              -           Siriel Shaid Mchembe
 2. Kilombero     -           James Mugendi Ihunyo
 3. Mvomero       -           Mohamed Mussa Utali
 4. Morogoro      -           Regina Reginald Chonjo
 5. Ulanga                        -           Kassema Jacob Joseph
 6. Kilosa             -           Adam Idd Mgoyi
 7. Malinyi           -           Majula Mateko Kasika

MTWARA
 1. Newala           -           Aziza Ally Mangosongo
 2. Nanyumbu    -           Joakim Wangabo
 3. Mtwara           -           Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
 4. Masasi                        -           Seleman Mzee Seleman
 5. Tandahimba -           Sebastian M. Walyuba

MWANZA
 1. Ilemela           -           Dkt. Leonald Moses Massale
 2. Kwimba          -           Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
 3. Sengerema     -           Emmanuel Enock Kipole
 4. Nyamagana    -           Mary Tesha Onesmo
 5. Magu              -           Hadija Rashid Nyembo
 6. Ukerewe        -           Estomihn Fransis Chang'ah
 7. Misungwi       -           Juma Sweda

NJOMBE
 1. Njombe          -           Ruth Blasio Msafiri
 2. Ludewa                      -           Andrea Axwesso Tsere
 3. Wanging'ombe          -           Ally Mohamed Kassige
 4. Makete                       -           Veronica Kessy

PWANI
 1. Bagamoyo      -           Alhaji Majid Hemed Mwanga
 2. Mkuranga      -           Filberto H. Sanga
 3. Rufiji               -           Juma Abdallah Njwayo
 4. Mafia              -           Shaibu Ahamed Nunduma
 5. Kibaha           -           Asumpter Nsunju Mshama
 6. Kisarawe        -           Happyness Seneda William
 7. Kibiti               -           Gulamu Hussein Shaban Kifu

RUKWA
 1. Sumbawanga -           Dkt. Khalfan Boniface Haule
 2. Nkasi              -           Said Mohamed Mtanda
 3. Kalambo        -           Julieth Nkembanyi Binyura

RUVUMA
 1. Namtumbo    -           Luckness Adrian Amlima
 2. Mbinga           -           Cosmas Nyano Nshenye
 3. Nyasa             -           Isabera Octava Chilumba
 4. Tunduru        -           Juma Homela
 5. Songea           -           Polet Kamando Mgema

SHINYANGA
 1. Kishapu         -           Nyambonga Daudi Taraba
 2. Kahama         -           Fadhili Nkulu
 3. Shinyanga      -           Josephine Rabby Matiro

SIMIYU
 1. Busega           -           Tano Seif Mwera
 2. Maswa                        -           Sefu Abdallah Shekalaghe
 3. Bariadi           -           Festo Sheimu Kiswaga
 4. Meatu             -           Joseph Elieza Chilongani
 5. Itilima             -           Benson Salehe Kilangi

SINGIDA
 1. Mkalama       -           Jackson Jonas Masako
 2. Manyoni        -           Mwembe Idephonce Geofrey
 3. Singida           -           Elias Choro John Tarimo
 4. Ikungi             -           Fikiri Avias Said
 5. Iramba           -           Emmanuel Jumanne Luhahula

SONGWE
 1. Songwe           -           Samwel Jeremiah
 2. Ileje                -           Joseph Modest Mkude
 3. Mbozi             -           Ally Masoud Maswanya
 4. Momba          -           Juma Said Irando


TABORA
 1. Nzega             -           Geofrey William Ngudula
 2. Kaliua             -           Busalama Abel Yeji
 3. Igunga                        -           Mwaipopo John Gabriel
 4. Sikonge          -           Peres Boniphace Magiri
 5. Tabora           -           Queen Mwashinga Mlozi
 6. Urambo         -           Angelina John Kwingwa
 7. Uyui                -           Gabriel Simon Mnyele

TANGA
 1. Tanga             -           Thobias Mwilapwa
 2. Muheza          -           Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
 3. Mkinga           -           Yona Lucas Maki
 4. Pangani          -           Zainab Abdallah Issa
 5. Handeni        -           Godwin Crydon Gondwe
 6. Korogwe        -           Robert Gabriel
 7. Kilindi                        -           Sauda Salum Mtondoo
 8. Lushoto         -           Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016