Friday, December 30, 2016

"Wakulima wanahitaji elimu ya kilimo chenye tija" Mh. Zelote StephenMkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen awaasa maafisa ugani wa kilimo kuyatumia vizuri mashamba darasa ili kutoa elimu ya kilimo ili kuleta kilimo chenye tija hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua wenye mashaka. 

Aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku mbili ya kuangalia utendaji kazi wa maafisa ugani akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Dk. Halfan Haule.

Mh. Zelote Stephen aahirisha ziara na kushiriki kwenye msiba wa mwanakijiji cha Mpui


Mh. Zelote Stephen awahamasisha wanamuze kujiunga na REA


Mh. Angeline Mabula aitahadharisha manispaa ya sumbawanga kuhusu migogoro ya Ardhi


Mh. Angeline Mabula atembelea mradi wa NHC sumbawanga


Mh. Zelote Stephen apokea ripoti ya hali ya kilimo katika H/W ya Sumbawanga


Monday, December 26, 2016

Mama Flora Zelote aungana na watoto yatima kusheherekea ChrismasMke wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mama Flora Zelote Stephen akiwa ameungana na wenzake, Mke wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Mama Grace Nzuda, mke wa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mama Teresia Haule na Mke wa Sumry, Naisara Hirah walishiriki katika kusherehekea sikukuu ya Kristmas na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Shirika la Mtakatifu Maria mama wa Afrika kilichopo katika kata ya Katandala, wilaya ya Sumbwanga.


Mama Zelote alisema kuwa kushiriki pamoja na watoto ambao hawana wazazi ni la kila mwanajamii ili watoto hawa wasijisikie wapweke hasa katika kipindi hiki ambacho watoto wenye wazazi wao wanakuwa na furaha.

"Tumeona ni jambo la muhimu kuwakumbuka hawa watoto ambao kwa iasi kikubwa wanajamii wengi wanakuwa wanajisahau kuwa kuna watoto aina hii ambao wanahitaji kuona nao wanajaliwa katika siku hizi za sikukuu na siku nyingine," Mama Flora Zelote alielezea.

Wake hao wa Viongozi walitoa zawadi ya Mbuzi mmoja, Jogoo, Mchele, Sabuni, Juice, na pampers za watoto wadogo ambavyo vina thamani zaidi ya Laki mbili. 
Mama Flora Zelote akiwakabidhi watoto zawadi ya Chrismas katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shirika la Mtakatifu Maria mama wa Afrika, kilichopo Katandala, Wilaya ya Sumbawanga  

Mama Flora Zelote akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha watoto Yatima cha Mama Maria  kilichopo Katandala, wilaya ya Sumbawanga


Mama Teresia haule akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho. 


Kutoka Kulia, Mama Mapugilo, Mama Teresia Haule, Mama Grace Nzunda, Bi. Naisara Hirah na Mama Flora Zelote 


Picha ya Pamoja na watoto


Picha ya Pamoja na watoto


Picha ya Pamoja na watoto

Picha ya Pamoja na watoto


Mama Flora Zelote akipeana Mkono na Sister Teresia mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shirika la Mtakatifu Maria mama wa Afrika.

Zawadi ya Mbuzi

Mh. Zelote Stephen Awapa pole na kuwatahadharisha wananchi kujenga nyumba Imara kuepuka maafa.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akielezea namna nyumba zilivyokuwa hazina uimara katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen amewatahadharisha wananchi wa mkoa wa Rukwa kujenga nyumba zenye kufuata taratibu za kitaalamu ili kuweza kuhimili mvua za upepo

Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipokwenda kutembelea na kuwapa pole wanakijiji wa kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga, waliopotelewa na nyumba zaidi ya Ishirini zilizoezuliwa paa pamoja na kuanguka kwa kuta za nyumba hizo.

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa mbali na kujenga nyumba imara lakini pia wananchi wanapaswa kuzingatia kupanda miti kwa wingi ili upepo upambane na miti kabla ya kukutana na nyumba.

"Ukiangalia nyumba nyingi zinajengwa kwa udongo wa kawaida bila ya kutumia udongo ulaya (cement), sasa hapa unakaribisha hatari na tofari zenyewe ni nzito sana, zinashikiliwa na udongo kidogo, halafu miti pia hakuna ambayo inazunguka nyumba ili kuweza kupambana na upepo mkali" Mkuu wa Mkoa alifafanua. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga.

Moja ya Nyumba iliyopata maaafa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga. 
Saturday, December 24, 2016

"Tuendelee kuvitunza vyanzo vya maji," Mh. Inj. Gerson Lwenge

Waziri wa maji Mh. Inji. Gerson Lwenge amewasisitiza wananchi kuendele kutunza vyanzo vya maji ili wananchi waendelee kuwa na maji ya kugawiana kadiri miaka inavyokwenda mbele.
Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, (kushoto), Waziri wa Maji Mh.Inj. Gerson Lwennge.

Picha ya Pamoja.
Aliyasema hayo baada ya Kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Kuonana na Mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika ziara yake ya siku mbili katika Mkoa.

Mh. Lwenge alisisitiza wananchi kutoendelea kufanya shughuli za kibinaadamu katika vyanzo vya maji na badala yake wapande miti kwa wingi ili kutunza mazingira.

Picha ya pamoja.
"Kuna utafiti umefanyika unaonesha kuwa kama itatokea vita ya tatu, basi watu watagombania maji, hata ukiangalia ugomvi wa wakulima na wafugaji chanzo ni ukosefu wa maji, mifugo imekosa maji na hatimae inaanza kuranda kutafuta maji mwishowe huingia kwenye mashamba na kusababisha ugomvi," Mh. Lwenge alifafanua


"Tuko mbioni kumalizia mahakama 10 za kisasa," Mh. Mohamed Chande Othman

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Cahnde Othman amesema Tanzania iko mbioni kumalizia ujenzi wa mahakama 10 za teknolojia ya kisasa, za ujenzi wa bei nafuu na zenye uimara ili ziwe za mfano. katika kutoa huduma kwa teknolojia ya kisasa.
Kutoka kushoto, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Otheman, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kanda ya Sumbawanga Mh. Mgeta, Mtendaji Mkuu wa watumishi wa Mahakama, Emanuel Munda.

Mh. Chande ameyasema hayo alipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika ziara yake ya siku mbili Mkoani hapa.

Katika ziara hiyo Mh. Chande amekiri kuwa mahakama zina mzigo mzito wa kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoa hukumu mapema ili wananchi wawe na imani na mfumo wa kupata haki zao.

Katika kusherehesha hilo Mh. Chande hakuacha kulishukuru jeshi la polisi kwa kuhakikisha upepelezi unamalizika mapema na pia aliupongeza MKoa wa Rukwa kwa kutokuwa na malalamiko mengi ya wahukumiwa kupata nakala zao za hukumu pindi tu hukumu inapofikiwa.
Kutoka kushoto, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Otheman, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kanda ya Sumbawanga Mh. Mgeta, 
Mh. Chande aliongeza kuwa pamoja na Tanzania kuwa na mahaka za mwanzo 960 ambazo zinashikilia asilimia 72 mashauri ya kesi za nchi nzima, bado mhimili wa mahakama unahitaji kupewa nguvu zaidi ili kuweza kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.

Jambo ambalo lilimfanya amsifu Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuweza kuliona hilo na kuwapatia shilingi Bilioni 12.3 ili kuweza kuanza kuimarisha mhimili huo.

Mh. Chande aliyazungumza hayo baaada ya kusikiliza risala fupi iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ambaye alielezea upungufu wa mahakimu katika mahakama za mwanzo jambo ambalo linapelekea ucheleshwaji wa kesi na kuleta hisia mbaya kwa wananchi na kuwafanya wahisi kesi ambazo hucheleshwa ni kwasababu ya rushwa."Nawatakia wanarukwa Heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2017, lakini....," Mh. Zelote Stephen

SALAMU ZA CHRISMASS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHESHIMIWA ZELOTE STEPHEN ZELOTE KWA WANANCHI WOTE WA MKOA WA RUKWA 

Ndugu Wananchi,
Tunapokaribia kumaliza Mwaka 2016 napenda nichukue nafasi hii kwa dhati na moyo mkunjufu kuwashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwamba amani na utulivu inatawala muda wote katika Mkoa wa Rukwa.  Ni imani yangu na matarajio yangu kwamba mwaka unaofuata Mwenyekzi Mungu akituvusha salama tutaendelea ama tutazidisha ushirikiano uliokuwepo.

Pili, nachukua nafasi hii kuwatakia sikukuu njema na baraka tele toka kwa Mwenyezi Mungu.  Katika siku hizo nawaomba kila mmoja asherehekee kwa mipaka yenye kujali amani, utulivu, kuzingatia sheria ikiwa ni pamoja na kulinda maisha na mambo mengine yote muhimu yanayotuzunguka.  Natumaini vyombo vinavyohusika kuhakikisha ulinzi na usalama ndani ya Mkoa vitavitimiza majukumu yake kwa weledi mkubwa. 

Ndugu Wananchi,
Katika Mwaka unaomalizika yapo mambo mengi tuliyoyafanya kwa ajili ya manufaa na maendeleo ya Mkoa wetu ndani yake kukiwemo lengo la kunyanyua maisha ya kila mwananchi kiuchumi.  Nawaomba sana tuendelee kushirikiana na Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye nia na dhamira ya hali ya juu ya kuleta mabadiliko kwa manufaa ya kila Mtanzania.  Binafsi nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa utumishi na uongozi wa namna ya pekee katika Taifa letu la Tanzania

Tumuunge mkono katika kupiga vita vitendo vya Rushwa, Ufisadi, Ubadhilifu na Kutowajibika ipasavyo kwa baadhi ya Watumishi wa Umma sehemu za kazi.  Naamini tukiungana naye tutafanikiwa kuondosha mambo yote hayo mabaya.  Vilevile napenda kuhimiza kila mtu ajitume kufanya kazi.

Ndugu Wananchi,
Kumekuwepo na matukio mbalimbali; wengine wamepoteza ndugu zao kwa matukio mbalimbali ikiwepo ajali, moto, hali ya hewa, maradhi na kadhalika.  Nachukua nafasi hii kuwapa pole.

Ndugu Wananchi,
Hali ya hewa ambayo ndio msingi tunaoutegemea sana kwa ajili ya kilimo katika Mkoa wetu inayumba.  Mvua hazinyeshi kwa kawaida yake.  Kutokana na hali hiyo natoa rai kama ifuatavyo:-

i.                   Wananchi watunze akiba ya chakula waliyojiwekea.  Kisitumika kwa kuuza ama kutengeneza pombe badala yake wahifadhi ili ituvushe kipindi ambacho kipo mbele yetu.
ii.                Sambamba na hilo natoa wito watu walime mazao yanayoweza kuhimili ukame mfano Viazi vitamu, Mihogo, Ulenzi na Mtama.  Naagiza Halmashauri zote kusimamia agizo hili.

iii.              Natambua kwamba Pembejeo za Ruzuku zilichelewa kidogo lakini jambo hilo limerekebishwa na usambazaji wa Pembejeo hizo unaendelea vizuri zoezi ambalo tunafuatilia kwa karibu sana.  Hata hivyo hata wale ambao sio wanufaika wa pembejeo hizo wamekuwa wakipata huduma hiyi katika maduka ya pembejeo za Ruzuku kwa bei ya kawaida.  Serikali inajitahidi kuhakikisha pembejeo hizo zinakuwa zenye ubora na sio feki.

Ndugu Wananchi,
Napenda nimalizie salamu zangu kwa kuwatakia wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa kila la Kheri kwa sherehe zote zijazo ikiwa ni pamoja na kuaga Mwaka wa 2016 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2017 katika hali ya Amani na Utulivu.

Asanteni kwa kunisikiliza


Zelote Stephen Zelote
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa


Mh. Zelote aagiza Nesi kuchukuliwa hatua baada ya kuwapuuza wagonjwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameagiza Muuguzi wa kituo cha Afya cha Mtowisa kuchukuliwa hatua baada ya kubainika kumpuuza majeruhi aliyeangukiwa na tofali na kupata michubuko katika maafa yaliyotokea katika kijiji cha Mwela Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga. 

Muuguzi huyo ambae inasemekana baada ya majeruhi hao kuwasili katika kituo hicho cha afya saa tano usiku wakihitaji msaada, yeye aliwaandikia dawa waende kutafuta katika dawa hizo katika maduka yaliyopo nje ya hospitali.

Mkuu wa Mkoa alifika katika kituo hicho cha afya baada ya kutoka kutoa pole kwa waathirika wa maafa ya Mvua yaliyoezua nyumba 24 ili kujihakikishia na kuona kuwa kuna dawa za kutosha na hakukuwa na sababu ya muuguzi huyo kuwaelekeza majeruhi hao katika maduka yaliyopo nje ya hospitali

“Huyu Nesi achukuliwe hatua, narudia kusema ni bora tubaki na muuguzi mmoja ambaye ni mwadilifu na anayetuwakilisha vizuri, Kwasababu hiki kituo hakikuwekwa kwa bahati mbaya kimewekwa kwaajili ya hawa wenye shida wanaokimbilia huku kupata huduma” Mh. Zelote Alisisitiza.

Mh. Zelote aliongeza kuwa muuguzi huyo anaweza kuwa ni miongoni mwa watumishi ambao hawatoi huduma mpaka mwananchi ajipapase na kutoa chochote.

Kaimu Mganga wa kituo hicho cha afya Dokta Thomas Cyprian alikiri kutokea kwa tukio hilo na kumuahidi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuwa kamati ya maadili ya kituo hicho kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule watakaa na kumchukulia hatua.


“Ni kweli baada ya mimi kupata taarifa za tukio hilo, nilimwita na kumuuliza na kweli alieleza kilichotokea kuwa ndivyo hali ilivyokuwa,” Dk. Cyprian alisimulia.


Mh. Zelote Stephen ameagiza duka la Dawa kufungwa baada ya Kugundua kuwa muuzaji hana sifa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameagiza duka la dawa hadi hapo muuzaji huyo atakapopata mafunzo ya ADO ili kuepusha madhara kwa wananchi anaowauzia dawa hizo.

Mh. Zelote aliagiza hayo baada ya kutembelea duka la dawa muhimu katika kijiji cha Mwela kata ya Mtowisa ambapo alitembelea watu waliopatwa na maafa katika kijiji hicho.

Duka hilo ambalo lilifanyiwa ukaguzi na watumishi kutoka Wizara ya Afya tangu tarehe 9.11.2016 nakubainika na makosa kadhaa ikiwemo muuza dawa hizo kutokuwa na sifa za kuuza dawa na “Shelf” za kuwekea dawa kutokuwa na ubora unaotakiwa, na kutolipia leseni ya mwaka 2016/2017.

Watumishi hao wa Wizara ya Afya waliagiza muuza dawa huyo kupelekwa kwenye mafunzo ya ADO, pamoja na kulipia leseni, na kurekebisha “Shelf”.
Makosa ambayo yalitakiwa kurekebishwa hadi kufikia tarehe 23.11.2016, lakini hadi Mh. Zelote anafika katika duka hilo, Muuzaji bado alikuwa anaendelea kutoa huduma bila ya kukamilisha agizo lolote kati ya maagizo yaliyotolewa na Wizara ya Afya.

Daktari Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Kabuga alithibitisha kuwa ukaguzi huo ulifanyika na maagizo hayo yalitolewa lakini hawakujua kama bado duka hilo linaendelea kutoa huduma.


Mmiliki wa duka hilo Bi. Leticia Mtama hakuweza kupatika na hatimae muuza duka kuachiwa maagizo ya kufunga duka hadi hapo atakapokamilisha maagizo hayo. 


Waziri Mkuu akagua Eneo la Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA

*Ni kufuatia agizo la Rais Magufuli wapewe sh. bilioni 10
*TBA kujenga nyumba 320, askari wafungwa kufyatua matofali
*Mkuu wa Magereza aahidi kuokoa fedha za kujenga nyumba nyingine 80

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kukagua eneo la ujenzi wa makazi ya askari wa Magereza unaotarajiwa kuanza baada ya wiki tatu zijazo.

Akizungumza na askari wa magereza kabla ya kufanya ukaguzi huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) Waziri Mkuu amesema ziara aliyoifanya leo, ni ufuatiliaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipoenda kukagua gereza hilo.

Novemba 29, mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara kwenye gereza hilo na kupokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo zipatazo 9,500 na akaagiza zitafutwe sh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Waziri Mkuu amesema amefarijika kukuta Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wako eneo la kazi na wameanza kusafisha eneo hilo.

“Nimefarijika kukuta TBA wako kazini na nimeelezwa hatua inayofuata ni upimaji wa sampuli za udongo kabla hawajaanza kujenga msingi. Nawapongeza TBA kwa kazi nzuri wanazofanya za ujenzi wa nyumba zenye viwango na kwa haraka kama tulivyoona kule Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyumba za Magomeni Kota,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango uliofanywa na Serikali ya awamu ya nne katika suala la makazi ya askari kama vile wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Polisi. “Nia ya Serikali ni kuhakikisha makamanda wote wanapata nyumba nzuri ili waendelee kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa wakiwa na uhakika familia zao zimetulia kwenye makazi bora”.

Amesema katika ziara alizozifanya kwenye mikoa mbalimbali, alitembelea magereza ya Isanga, Msalato (Dodoma), Lindi, Singida na Keko (Dar es Salaam) alikuta nyumba za askari hazina viwango na kama zipo zimechakaa sana.

Mapema, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa nyumba hizo, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa makazi ya askari na kwamba jeshi hilo litafanya kazi zote zisizo za kitaalamu ili kuokoa fedha za Serikali na badala ya kulipwa watu binafsi, fedha hizo zitatumika kuongeza nyumba zaidi.

“Tumekubaliana na TBA kazi zote zisizohitaji utalaamu kama kufyatua matofali, kubeba mizigo au kufyeka zitafanywa na askari wetu pamoja na wafungwa ili tuokoe gharama zote hizo na badala ya kulipa watu binafsi, fedha hizo zitumike kujenga nyumba nyingine 80,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema wamejipanga kufanya kazi hizo kwa saa 24 kila siku ili kuokoa muda ambao TBA walikuwa wameuweka wa kukamilisha ujenzi ndani ya miezi minane.

Alisema wako tayari kuanzisha kambi za ujenzi kwa kutumia wafungwa na askari ili wafanye kazi zisizohitaji utaalamu na fedha zitakazopatikana, badala ya kuwalipa watu binafsi zitumike kujenga nyumba zaidi za askari.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Bw. Baltazar Kimangano alisema wanataraji kuanza ujenzi ndani ya wiki tatu baada ya kupokea matokeo ya uchunguzi wa sampuli za udongo kutoka taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema wanataraji kujenga majengo (block) manne ya ghorofa sita kila moja ambayo kwa ujumla yatakuwa na nyumba 240 zenye ukubwa wa vyumba viwili vya kulala. Pia watajenga majengo (block) mengine mawili ya ghorofa sita kila moja ambayo yatakuwa na nyumba 80 zenye ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala.

(mwisho)    
                            
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM
JUMAMOSI, DESEMBA 24, 2016.

Mama Majaliwa atoa Misaada kwa Yatima

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAMA MAJALIWA ATOA MISAADA KWA YATIMA

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa makundi ya watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mama Majaliwa ametoa msaada huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo vitatu vya CHAKUWAMA kilichopo Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na CHAMAZI kilichopo Mbagala.

Akikabidhi msaada huo ikiwemo mchele, sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa amesema ameona ni vema atoe msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine.

Pia ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa kusaidia makundi yenye uhitaji.

Kwa upande wao, walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima vya CHAKUWAMA na HISANI wamemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo huku baadhi ya watoto wakisema msaada huo umewapa faraja kubwa.

Mlezi wa kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada huo, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu za kuendelea kuwatumikia vizuri Watanzania.

Naye Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya Mutalemwa ameiomba jamii iendelee kuyakumbuka makundi yenye uhitaji kwani bado yanakabiliwa na changamoto nyingi za kufanikisha ndoto zao ikiwemo kupata elimu.

(mwisho)    
                            
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, DESEMBA 24, 2016.

Sunday, December 18, 2016

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa yawaaga wastaafu 8 tarehe 16/12/2016


John William Gurisha
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1984 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 32. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.


Anna Komba
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 38. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.


Daniela Leguna
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1982 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 34. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.


Leonard Chokola
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1982 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 34. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.

Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa, Lubinus Mgonya (kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda (katikati) na Katibu Tawala Utawala na Utumishi bora. Aboubakar Kunenge (kushoto) 

Bi. DAniela Leguna akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda.

Picha ya Pamoja

picha ya pamoja na wanafamilia za wastaafu

Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa Rukwa

Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa Rukwa

Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa Rukwa


Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa Rukwa


picha ya pamoja ya wastaafu walioagwa 

watoa burudani

wakati wa maakuli

watumishi a wageni mbalimbali wakiendelea kupata chakula

Lubinus Mgonya, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa akigonga "cheers" na Leonard Chokola wakati wa maagano hayo.


Wastaafu wengine ni

Philip Kapufi
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1982 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 34. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.

Emmy Godfrey
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 38. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.

Triphonia Itala
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 38. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.

Juliana Kaswende
Alianza kuitumikia serikali ya Tanzania mwaka 1975 hadi mwaka 2016 kwa muda wa miaka 41. Serikali ya Tanzania inakupongeza sana kwa utumishi wako na inakutakia maisha mema na afya njema.