Saturday, September 30, 2017

RC Rukwa awatahadharisha wananchi kujiandaa na msimu wa mvua

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewatahadharisha wananchi wa Mkoa huo kujihadhari na mvua  zilizoanza na upepo ulioezua baadhi ya paa za nyumba na vituo vya kutolea huduma katika baadhi ya maeneo ya mkoa.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliposhiriki kwenye usafi wa mwisho wa mwezi 30.9.2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliposhiriki kwenye usafi wa mwisho wa mwezi 30.9.2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliposhiriki kwenye usafi wa mwisho wa mwezi 30.9.2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliposhiriki kwenye usafi wa mwisho wa mwezi 30.9.2017

Amesema kuwa sasa ni wakati wa wazazi kuwachunga watoto katika msimu huu wa mvua na kuongeza kuwa wenye nyumba hawanabudi kuimarisha majengo yao mapema ili kuepukana na hasara ambayo wangeweza kuipata baada ya madhara kutokea.

“Ni wakati muafaka hivi sasa kila mtu kuchukua tahadhari kuangalia watoto, kukagua majengo yetu kuona kuwa yapo imara na pale ambapo ninatokea basi wajue sehemu salama ya kukimbilia ili kuokoa Maisha,”alifafanua

Ameyasema hayo aliposhiriki kufanya usafi nyumbani kwake eneo la Mkoani, mjini Sumbawanga. Ambapo alisema kuwa suala la usafi linaanzia nyumbani kwa mtu na kuwa wananchi wafanye usafi kwa faida yao wenyewe na kuendelea kuwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kusimamia usafi kuanzia ngazi ya Kijiji au mtaa ili kutekeleza agizo lake la kufanya usafi kuanzia katika ngazi hizo.

“Nimewaagiza wakurugenzi na wataalamu wake wakague usafi kwasababu suala la usafi ni faida kwa kila mtu, siyo faida ya rais wa la mkuu wa mkoa pekee, kwasababu tukiingiliwa na magonjwa halitakuwa la rais peke yake,” Alisema

Pamoja na hayo Mh. Zelote aliwaonya wenye tabia ya kuchoma misitu hasa katika kipindi hiki cha kukaribia msimu wa kilimo, hivyo amewasisitiza viongozi kuanzia ngazi ya Kijiji kushirikiana kuhakikisha kuwa jambo hilo halijitokezi.


“Katika kipindi hiki uchomaji hovyo wa mioto unaonekana kushika kasi, ni juu ya serikali ya Kijiji ama kata kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mioto haiwashwi ovyo ovyo na atakayefanya hivyo achukuliwe hatua za kisheriakwani mambo haya huaribu mazingira na pia usipodhibitiwa hule madhara,” Alisisitiza. 

Rc Rukwa apongeza juhudi za wanafunzi wa Mlimani kufanya utafiti wa uhun...

Wahasibu waaswa kufanya kazi kwa uadilifu

Katibu tawala msaidizi serikali za mitaaa wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya amewaasa watumishi wapya wa kada wa uhasibu katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria, taratibu na miongozo inayotolewa ili kuwaepusha kufanya kazi kwa mazoea.
Katibu tawala msaidizi serikali za mitaaa wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya 

Ameyasisitiza hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya uhasibu katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma (FFARS) akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
baadhi ya washiriki wa mafunzo

baadhi ya washiriki wa mafunzo

baadhi ya washiriki wa mafunzo

“Ni matumaini yangu kuwa baada ya mafunzo haya mtakuwa mmejenga uelewa wa kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka mbalimbali,” Alisema.

Aidha mafunzo hayo yamelenga kuwaboreshea ujuzi na stadi za kazi ikiwemo dhana ya kwenda na mahitaji ya wakati kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Technolojia.

Mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waajiriwa wapya wahasibu wasaidizi katika halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Sumbawanga vijijini, Nkasi na Kalambo, walioambatana na maafisa utumishi pamoja na maafisa takwimu wa Halmashauri hizo.


Pamoja na mafunzo hayo watumishi hao wapya walipata fursa ya kueleimishwa kuhusu mifuko mbalimbali ya jamii ikiwemo, PSPF, LAPF, NSSF, na mfuko wa bima ya afya wa Taifa (NHIF) ili kuwapa nafasi watumishi hao wapya kuamua kwa hiari bila ya kulazimishwa mfuko ambao watapenda kujiunga. 

"Kupima maleria ni bure, TB Bure" Mh. Ummy Mwalimu akiwa Kirando

Tuesday, September 19, 2017

RC Rukwa atoa siku 7 kupatiwa orodha ya boti na mitumbwi mwambao wa ziwa Tanganyika.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametoa siku saba kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Kalambo pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kumpatia orodha kamili ya vyombo vyote vya majini vinavyofanya shughuli zake katika mwambao wa ziwa Tanganyika katika Wilaya za Nkasi na Kalmbo za Mkoa wa Rukwa.
Miongoni mwa mitumbwi iliyokuwa imezagaa katika mwambao wa ziwa Tanganhyika Kijiji cha Wampembe ambayo mingi haikuwa na usajili na kuipotezea serikali mapato katika sekta ya uvuvi.

Ametoa agizo hilo alipotembelea mwambao wa Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Wampembe, Kata ya Wampembe Wilaya ya Nkasi na kubaini mitumbwi kadhaa iliyokuwa ikizagaa kwenye mwambao huo ikiwa haijafanyiwa usajili na kusababisha upotevu wa mapato ya serikali kupitia sekta hiyo ya uvuvi.

“Halmashauri zimekuwa zikilalamika hazina mapato ya kutosha wakati naona pesa zikielea tu hapa na Hakuna chochote kinachoendelea, sasa natoa siku saba kwa Halmashauri na SUMATRA nipate orodha kamili ya vyombo vyote vya usafiri wa majini, usajili wao na leseni zao zinazowaruhusu kufanya shughuli za uvuvi katika mwambao huo.” Amesema.
Mmoja wa maafisa wa Sumatra (mwenye overoli la bluu) akitoa ufafanuzi mbele ya Mh. Zelote (mwenye kaunda suti0 pamoja na maafisa mbalimbali walioambatana katika ziara hiyo kwenye kijiji cha Wampembe, Wilayani Nkasi.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen (kushoto) akimuonesha Afisa Uvuvi wa Kata Godfrey kashengebi (kulia) nyavu zilizobainika kutokidhi vipimo vilivyokubalika na serikali katika shughuli za uvuvi na kuagiza kukamatwa kwa kokoro hizo zilizokuwa zikiendela kutumiaka bila ya kukaguliwa na afisa huyo.

vijana wakiwa wamebeba kokoro zilizoagizwa kukamatwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa na kufikishwa ofisi ya kata. 

Pamoja na hayo agizo hilo pia limekuja baada ya wiki moja iliyopita boti ambayo mmiliki wake hakujulikani kuzama ziwa Tanganyika ikitokea katika Kijiji cha Kalila, Kata ya kabwe, tarafa ya Kirando, Wilayani Nkasi  kuelekea Kijiji cha Kyala Mkoani Kigoma na kupelekea kifo cha mtoto mmoja na watoto wengine wawili kuhofiwa kufa maji huku watu 11 wakiokolewa. Na wafanyakazi wawili wa boti hiyo kukimbia.

Katika kuhakikisha usalama wa Kijiji cha Wampembe unaimarika Mh. Zelote aliagiza kuhamishwa kwa watumishi wawili, Afisa Mtendaji wa kata ya Wampembe Faustine Wakulichamba pamoja na Afisa uvuvi wa Kata Godfrey Kashengebi kwa makosa mbalimbali moja ikiwa kutosimamia makusanyo ya mapato ya uvuvi jambo lililopelekea kudorora kwa makusanyo ya mapato  pamoja na kuwepo kwenye kata hiyo kwa miaka zaidi ya sita jambo ambalo linapunguza ufanisi wao wa kazi.

Katika doria hiyo Mh. Zelote pia alikamata kokoro na nyavu kadhaa zilizokuwa hazikukidhi vipimo vya serikali katika matumizi yake jambo ambalo maafisa hao walifumbia macho na kuisababishia serikali upotevu wa mapato.


Kwa mujibu wa sheria za halmashauri mtumbwi wenye urefu wa mita 4 hulipiwa dola 4 kwa mwaka kama ada ya usajili. 

RC Rukwa atoa Siku tatu kuhakikisha huduma ya upasuaji inapatikana Wampembe

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameipa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi siku tatu kuhakikisha kuwa wanafanya marekebisho ya mfumo wa maji unaohudumia kituo cha afya cha Wampembe jambo ambalo linakwamisha huduma ya maji katika kituo hicho.

Ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya ghafla katika kituo hicho ili kuona utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa tangu kuanza kwa mwaka huu, ziara hiyo ya siku tatu ililenga kuangalia utekelezaji katika sekta ya elimu, afya, maji, na uwekezaji wa viwanda.

Katika kuhakikisha jambo hilo linakamilika aliagiza mhandisi wa maji wa Halmashauri hiyo Eric Namakonde ambaye aliambatana na msafara huo kubaki siku hizo na kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika na kupatiwa ripoti.
Mkuu wa Mkoa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa kaunda suti) akitoa maelekezo juu ya urekebishaji wa mfumo wa maji kutoka ziwa tanganyika kwenda katika kituo cha afya Wampembe. 

“Nimekuja mwezi wa tano na kuagiza hili jambo likamilike mpaka sasa sioni kinachoendelea, huwa sipendi kurudia maagizo sasa mhandisi wa maji ubaki hapa hadi marekebisho yakamilike na taarifa inifikie mezani ndani ya siku tatu,” Amesema

Kijiji cha Wampembe kipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, Wilaya ya Nkasi na kutoka makao makuu ya wilaya hadi katika Kijijini hapo ni kilomita 117 umbali ambao unasababisha hali mbaya kwa wananchi ambao wanataka kufanyiwa upasuaji katika kituo hicho ambacho kina maabara iliyokamilika ila inakosa huduma ya maji tu, na gharama ya marekebisho ya uharibifu Shilingi 800,000/=.

Mabomba (yaliyolala) yaliyofanyiwa uharibifu na kusababisha kushindikana kupandisha maji kutoka ziwa Tanganyika kuelekea katika kituo cha Afya Wampembe kilichopo kwenye mwambao wa Ziwa hilo


Mhandisi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Shabani Daudi (mwenye sati jekundu) akitoa ushauri juu ya kuimarisha mfumo wa maji utakaosadidia upatikanaji wa maji katika kituo cha afya Wampembe. 

“Msafara huu ambao nimekuja nao, si ushafikia hiyo gharama tayari, sasa mnataka tuwe tunakuja huku kila siku kwaajili ya jambo hili tu, sasa sitaki kurudi huku kwa jambo hili tena,” Amesema.


kwa muda wa miaka miwili wananchi wamekuwa wakilazimika kuchota maji katika visima vilivyopo Kijiji hapo na kufikisha kituoni hapo pindi ndugu yao anapotaka kufanyiwa upasuaji jambo ambalo Mh. Zelote hakukubaliana nalo. 

Kikongwe kupatiwa kiwanja karibu na Ikulu ndogo halmashauri ya Nkasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kumtafutia kiwanja cha nyumba Bibi Georgina Kapilima ili waweze kujenga nyumba na kuishi bila ya bughudha.
Ushauri huo umetolewa baada ya bibi huyo kumuomba Mkuu wa Mkoa katika siku maalum ambayo Mkuu wa Mkoa aliiweka maalum kwaajili ya kusikiliza kero na maombi mbalimbali ya wananchi ambao walijitokeza kuzungumza moja kwa moja na Mkuu huyo.

Bibi huyo ambaye alianza kwa kuilaumu Halmashauri hiyo baada ya kufika katika ofisi hizo mara kadhaa akidai kutafutiwa kiwanja cha kununua baada ya kuona majumba yakiendelea kujengwa katika mji huo unaoendelea nae akiumia kwa kulipa kodi ya shilingi 45,000 kwa miezi mitatu, jambo ambalo linamuweka katika wakati mgumu kutafuta pesa ya kodi hiyo.

“Ombi la huyu bibi ni la msingi sana, maana kila kukicha anaona nyumba zinamea tu lakini yeye akihitaji kiwanja anaambiwa hakuna jambo ambalo halimuingii akilini, kwahiyo Mkurugenzi, na Katibu tawala fanyeni utaratibu huyu bibi apatiwe kiwanja aweze kujenga nyumba,” Mh. Zelote alieleza.
Bibi Georgina Kapilima akisikiliza maamuzi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (hayupo pichani) mara baada ya kutoa malalamiko yake juu ya kukosa kiwanja cha kununua ili ajenge nyumba.

Awali alipokaribishwa kueleza shida yake mbele ya Mkuu wa MKoa Bibi Kapilima mwenye miaka 60 alisema kuwa kila akifika ofisi za halmashauri kuomba kiwanja anaambiwa hakuna huku akiona watumishi wa halmashauri hiyo wakiendelea kujenga majumba na kuongeza kuwa hataki kiwanja hicho bure na kuwa yupo tayari kukilipia ili nae awe na kwake. 
  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (katikati kwenye meza kuu) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi na Katibu tawala wa Wilaya juu ya kushughulikia tatizo la Bibi Georgina Kapilima.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (katikati) akitoa ufafanuzi wakati alipokuwa akisikiliza kero na maombi mbalimbali ya wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, kuliani kwake ni Katibu tawala wa Wilaya ya Nkasi Festo Chonya na Kushotoni kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa H/W ya Nkasi Abel Mtupwa.

Kwa kulipatia ufumbuzi jambo hilo katibu tawala wa Wilaya ya Nkasi Festo Chonya alitoa ahadi ya kumpatia kikongwe huyo moja ya viwanja 35 vilivyopo karibu na ikulu ndogo ya Wilaya ya Nkasi, Mjini Namanyere.

Mbali na kikongwe huyo Mh. Zelote alisikiliza kero za wananchi 14 kwa siku hiyo na kuweza kuzipatia ufumbuzi na wananchi hao kuondoka wakiwa wameridhika na maamuzi ya Mkuu wa Mkoa katika kutatua kero zao hizo.


Katika kusikiliza kero hizo Mkuu wa mkoa alikuwa na wakuu wa Idara za halmashauri hiyo, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilay pamoja na baadhi wa wakuu wa idara kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

“Kukamata na kuchoma nyavu haitoshi, tuwachome wahalifu” RC Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafi Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Kulia)akitoa
maelekezo namna ya kuziteketeza nyavu haramu (hazimo kwenye picha) mbele ya
maafisa aliongozana nao kushiriki uteketezaji wa zana hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Katikati
Mwenye suti ya ugoro) akiwasha moto tayari kwaajili ya kuzitekezeteza zana
haramu, kulia ni Juma Makongoro Afisa Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa
kushoto ni diwani wa kata ya kirando Kessy Sood

Nyavu zenye thamani ya shilingi milioni 57.6 zikiteketezwa

Kamishna Mstaafu Zelote amesema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, Mandakerenge, Kolwe, Lupata na Kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo, zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando. 
"Kukamata na kuchoma nyavu haitoshi kwa sababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria. Nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea mazingira yanaharibika. Sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa Mahakamani na kupewa adhabu," amesema Kamishna Mstaafu Zelote.
Mhe. Zelote amewaasa watumishi wa idara ya uvuvi ambao wapo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuachana na kupokea rushwa, kwani jambo hilo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwa ajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.
Mhe. Zelote amesema kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa kutunza rasilimali na kujulishwa kwamba rasilimali hizo ni za watanzania wote ili waweze kuachana na tabia ya kuvua samaki kwa kutumia zana zisizokubalika.
Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pamoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi Septemba 2017 waliweza kukamata nyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.
Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8 mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Monday, September 11, 2017

Mwana Rukwa alamba Milioni 50 za Biko

Bilioni 7 kutumika kujenga chuo cha VETA Rukwa

Ili kufikia Tanzania ya Viwanda elimu ndio uti wa mgongo utakayoifanya Tanzania kufikia azama yake hiyo, hivyo Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kupitia chuo cha elimu ya Ufundi (VETA) imetenga shilingi Bilioni 7 kwaajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi katika Mkoa wa Rukwa.Akifafanua hayo mtafiti mwandamizi wa masoko ya ajira Julius Paulo Mjelwa amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho unategemewa kuanza mwezi wa 9/2017 na kabla ya kukifungua rasmi chuo hicho hupita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kuonana na watendaji wa mkoa ili kujua mahitaji ya mkoa husika katika fani mbalimbali za ufundi.

Hivyo alikutana na watendaji wa ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na halmashauri zake wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Bernard Makali na kuorodhesha maseomo ambayo wanategemea kuyafundisha mara tu chuo kitakapoanza kufanya shughuli zake.

Masomo waliyopanga kuyafundisha ni pamoja na ufundi wa magari, uchomeleaji vyuma, huduma za vyakula na vinywaji, umeme wa majumbani, usindikaji wa vyakula, ushonaji, ukatibu muktasi, useremala pamoja na ujenzi. Na chuo hicho kitajengwa katika eneo la msitu wa Muva, wilayani Sumbawanga kwa msaada wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika 

RAS Rukwa asisitiza kutolewa elimu sahihi ya Ushirika kwa wananchi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Benard Makali amewasisitiza wanakamati ya elimu na maendeleo ya ushirika ya  mkoa kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ya kufikisha elimu ya ushirika kwa wananchi ili iwanufaishe katika maisha yao ya kila siku.

Ameyasema hayo alipokuwa akiziindua kamati hiyo yenye wajumbe 10 kutoka katika halmashauri za Mkoa na sekta binafsi ili kuimarisha utendaji kazi na kuhakikisha kuwa leimu hiyo inasambazwa katika ngazi zote.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali (katikati waliokaa) Kuliani ni Afisa ushirika wa Mkoa, Wallace Kiama na Kushotoni ni Mhadhiri kutoka Chuo cha Ushirika Moshi, Novatus Wezarubi katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Elimu na maendeleo ya Ushirika ya mkoa wa Rukwa. 

“Hii ndiyo kamati ambayo itafufua ushirika, watu wakishaelewa maana ya ushirika watajiunga kuanzia maofisini hadi mitaani kuna watu ambao wngependa kujiunga lakini hawana elimu ya kustosha juu ya dhana ya ushirika,” Makali alisema.


Amewataka kuwa makini na vyama vinavyomea na hatimae kuwa na idadi kubwa bila ya kufanya kazi, hali inayoonyesha mpaka sasa mkoa una idadi ya vyama 166 na vinavyofanya kazi ni vichache na kuongeza kuwa vyama vinavyoendeshwa kwa ufanisi ndio vinavyohitajika na sio wingi wake.

Awali alipokuwa akisoma risala kwa mgeni rasmi, afisa wa ushirika wa Mkoa, Wallace Kiama alitaja baadhi changamoto zinazowakabili ikiwamo vitendea kazi pamoja na upungufu wa watumishi hasa katika ngazi ya halashauri jambo ambalo linawafanya kushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Katika kulijibu hilo katibu tawala wa Mkoa amesema kuwa anazitambua changamoto hizo na kuahidi kuzishughulikia kwani baadhi ya changamoto hizo zipo ndani ya uwezo wake na kuwataka ili elimu hiyo iwafikie wananchi kwa haraka waandae mada hiyo ambayo atawahitaji kuiwasilisha katika vikao vya maendeleo vya mkoa.


Zaidi ya hayo aliitaka kamati hiyo kuhakikisha kuwa vyama vyote vinaendeshwa  kwa kufuata sheria na kanuni za vyama vya Ushirika kwa ajili ya ufanisi.

Thursday, September 7, 2017

"Tulinde vyanzo vya maji, na Kalambo Falls tutaitangaza tu," Prof. Maghembe

RC alipotembelea banda la SAGCOT

Hiki ndio chakula cha asili cha kifipa

MUST wamuonesha RC Rukwa mashine ya kubembeleza mtoto

RC Rukwa awa Mgeni Rasmi Nane Nane Mbeya

Nane nane Manispaa ya Sumbawanga ilivyofana

RC Rukwa apewa Ushauri na Mtoto Lightness

RC Rukwa awashauri John Deere Nane nane Mbeya

Hotuba ya RC Nane Nane SMC

RC Rukwa atembelea Balton na Agro Meru Nane Nane Mbeya.

Tuesday, September 5, 2017

14 Waliokata mikono ya Albino wafungwa miaka 20 jela kila mmoja - Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameisifu mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga kwa kutimiza wajibu wake kisheria kwa kutoa hukumu ya miaka 20 jela kwa waliohusika kwenye kuwakata mikono watu  wenye ulemavu wa Ngozi.

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi na wasio na ulemavu huo watambue kuwa Sheria inawalinda na ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa wananchi wake wanakuwa salama muda wote na kusisitiza kuwa si kweli kwamba watu wenye ulemavu wa Ngozi hawapewi ulinzi wa kutosha na kwa kupitia kesi hizi wajue kuwa Sheria inawalinda na waendelee kuwa na Imani.
Mtoto Mwigulu Matonange  akiwa hospitali akiuguza majeraha baada ya kufanyika kitendo cha Kikatili na wenye imani za kishirika za kutaka utajiri kupitia viungo vya wenye ulemavu wa ngozi. 

Pia amewaonya wananchi wenye tabia ya kujichukulia sharia mikononi kwa kuwataka kushirikiana na vyombo vinashughulika na kutoa haki nchini kwa kutoa ushahidi pale unapohitajika.

“Kuna wananchi wanapenda kujichukulia sharia mikononi jambo hili halifai cha muhimu ni kuripoti na kama kuna ushahidi unahitajika basi ni jukumu lao kuvisaidia vyombo vya usalama kupata ushahidi huo ili haki itendeke kama ilivyokuwa kwenye hukumu ya kesi hizi , jambo ambalo limepewa kipaumbele ni ushahidi” Amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mawakili wanne waliokuwa wakiwatetea watuhumia ambao ni Bartazar Chambi, Charles Kasuku, Peter Kamyalile na Mathias Budodi 

Pia aliwasifu mawakili wa pande zote mbili kwa kutimiza kazi yao nzuri ya kuhakikisha kwamba haki inapatikana na kuwaomba waendeleze kasi hiyo ya kuzingatia weledi katika majukumu yao.

Aidha alitumia nafasi hiyo Kuiomba mahakama kushughulikia maovu yote isiwe tu ya kesi za wenye ulemavu wa ngozi lakini pia wala rushwa, wabadhirifu wa mali ya umma, wakwepaji wa kulipa kodi.

Hukumu ya Kesi ya Kwanza

Kesi hii namba 1/2015 iliyosomwa na Mheshimiwa Jaji Mkuu Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam Mambi Ilimhusisha mtoto Mwigulu Magesa Matonange mwenye umri wa miaka 7 aliyevamiwa alipokuwa akichunga ng’ombe na kukatwa kiungo cha mkono wa kushoto na watuhumiwa kutoweka na kiungo hicho katika Kijiji cha Nsia, Tarafa ya Mtowisa, wilayani Sumbawanga Februari 15, 2013.
Mwigulu Matonange akiwa na mkono wa bandia aliopatiwa baaya kupelekwa Marekani kupata huduma hiyo. 


Watuhumiwa hao walitoweka na kiungo hicho na hatimae walikamatwa na polisi Aprili 20, 2013 mkoani Tabora wakiwa katika harakati za kutafuta mnunuzi.

Kesi hiyo ilijumuisha watuhumiwa 10 ambao sita kati yao walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kila mmoja na wengine wanne kuachiwa baada ya mahakama kukosa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa hao.

Washtakiwa sita kati ya kumi waliokutwa na hatia ni Ignas Sungura, James Paschal, Ibrahim Tela, Faraja Jailos Mwezimpya, Weda Mashilingi na Nickson Ngalamila. 

Walioachiwa ni Kulwa Mashilingi, Peter Said Msabato, Hamis Rashid Manyanywa na James Patrick Ngalamila.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Dk.Adam Mambi alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi wa kiungo uliotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi 12 wakiwamo daktari na mkemia.
        
Jaji Mambi alisema Mahakama imejielekeza katika mambo kadhaa ya msingi ili kuthibitisha makosa hayo; iliangalia ushahidi wa mazingira; kitendo cha washitakiwa kukutwa na kiungo cha binadamu wakitafuta soko; na nia ovu ya kutenda kosa na kusababisha maumivu makali au kifo.

Alisema kosa la kula njama ya kuua, adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 215 ya kanuni ya adhabu sura 16, huku kosa la kufanya jaribio la kutaka kuua adhabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 211 ya kanuni ya adhabu sura 16 na kosa la kusababisha ulemavu wa kudumu adahabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 222 ya Kanuni ya adhabu sura 16.

Hukumu ya Kesi ya Pili

Kesi hii namba 46/2015 iliyosomwa na Mheshimiwa Jaji Mkuu Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam Mambi ilimhusisha Maria Chambanenge (39) Kijiji cha Mkowe, Miangalua, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoa wa Rukwa.
Maria Chambanenge 

Tukio hili lilitokea usiku wa 11/2/2013 chumbani kwake akiwa amelala na wanawe, Maria ni albino na haoni vizuri. Sasa ameongezewa ulemavu wa viungo. Huyu ni mama wa watoto wanne: Shukuru (8), Edron (6), Rahab (3) na Emma (miezi mitano). Mama huyu ni mke wa tatu wa Gabriel Yohana.

Maria Chambanenge akipatiwa huduma. 
Maria alieleza namna ilivyotokea “Usiku wa manane, kati ya saa saba na saa nane hivi, Nilisikia vishindo vya nyayo vikitokea sebuleni ambako mwanangu Shukuru na Edron walikuwa wamelala. Ghafla nikamwona mume wangu ameshika upanga ananishambulia kichwani. Nikawa nashangaa na kuwaangalia usoni bila kujua kwa nini alikuwa ananishambulia. Akasema, “Nyamaza!” Mimi nikawa nalia. Akasema, Pole!  Nyamaza!”

Watuhumiwa walishtakiwa kwa makosa matatu kula njama ya kuua, jaribio la kuua mtoto mlemavu wa ngozi na kumsababishia ulemavu wa kudumu.

Watatu kati ya watuhumiwa 4 wa kesi hiyo ambao ni pamoja na Michael Kazanda na Linus Silikala Selemani walipewa kifungo cha miaka 20 kila mmoja kwa kosa la pili na la tatu na miaka 14 kwa kosa la kwanza.

Ntogwa Cosmas alikutwa na kosa la kwanza la kula njama za mauaji baada ya kushiriki kwa njia ya mawasiliano bila ya kuwepo eneo la tukio na kumsababishia kupewa kifungo cha miaka 14 na Frank Bernard kuachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha ushahidi usiopingika.

Jaji Mambi alisema Mahakama imejielekeza katika mambo kadhaa ya msingi ili kuthibitisha makosa hayo; iliangalia ushahidi wa mazingira; kitendo cha washitakiwa kukutwa na kiungo cha binadamu wakitafuta soko; na nia ovu ya kutenda kosa na kusababisha maumivu makali au kifo.

Alisema kosa la kula njama ya kuua, adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 215 ya kanuni ya adhabu sura 16, huku kosa la kufanya jaribio la kutaka kuua adhabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 211 ya kanuni ya adhabu sura 16 na kosa la kusababisha ulemavu wa kudumu adahabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 222 ya Kanuni ya adhabu sura 16.

Hukumu ya Kesi ya 3

Kesi hii namba 39/2016 iliyosomwa na Mheshimiwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga John Samwel Mgeta ilimhusisha mtoto Baraka Cosmas mwenhye umri wa miaka 6 anayeishi na wazazi wake kijijini Kipeta, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga ameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha mkono wake wa kulia.
Baraka Cosmas baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. 

 Tukio hilo la kikatili lilitokea saa saba usiku wa tarehe 12/3/2015 na wakati hayo yakitokea baba mzazi wa mtoto huyo inadaiwa alikuwa amelala katika nyumba ya mkewe mdogo kijijini humo. Na baadaye mtoto huyo alipelekwa kulazwa katika Kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani Mbeya kwa matibabu akiwa pamoja na mama mzazi.

Mama mzazi Prisca Shaaban Mpesya (28), mkazi wa Kitongoji cha Kikonde, Kijiji cha Kaoze katika Kata na Tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, alisema tukio hilo lilimkutana saa saba usiku, wakati akitaka kutoka nje kujisaidia.

 “Nilikuwa natoka nje kwenda kujisaidia, sijui ilikuwa saa ngapi kwa sababu sikuwa na saa, nje juu ya mlango tuliweka taa ya Mchina ya solar ambayo ilikuwa inaangaza, hivyo sikuwa na hofu,” akihadithia wakati alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Prisca Shabani Mama wa Baraka Cosmas akipatiwa huduma Hospitalini. 

Anasema ghafla tu alipofika mlangoni akashtuka kuona mtu akija mbio, akaipiga taa na kuivunja, kukawa giza.

“Nikajua huyu hakuwa mwema, hivyo nikajiandaa kupambana naye, alikuwa mwanamume mwenye nguvu kunishinda, lakini nilimdhibiti kwa sababu alitaka kuingia ndani kwa nguvu nami sikutaka kwa sababu wanangu walikuwa wamelala chini angeweza kuwaumiza.

“Mara nikasikia kitu kikinipiga kichwani pa! Nikaanguka na kupoteza fahamu. Nilipozinduka nikamwona mwanangu Baraka analia, kitanga cha mkono kimekatwa.” Akaongeza: “Natamani watu wanaofanya mambo haya wauawe hadharani.”

Anasema, mumewe Cosmas Yoramu Songoloka hakuwepo kwani alikuwa ameaga tangu mchana kwamba anakwenda kilabuni kunywa pombe, na mpaka majira hayo hakujua kama alikuwa kilabuni ama alikwenda kwa mke mdogo ingawa haikuwa zamu yake.
Jitihada za kupata tiba katika kituo cha afya Kamsamba wilayani Sumbawanga zilishindikana, hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Prisca ni mama wa watoto watatu wenhye ulemavu wa Ngozi na wakati tukio hilo likitokea alikuwa na mimba ya mtoto wa tatu na pia alikuwa na binti mdogo Lucia mwenye umri wa miaka 3 ambaye pia ni mlemavu wa Ngozi. Na Baraka (6) na wa kwanza anaitwa Shukuru (8) ambaye yeye si mlemavu na alimuacha nyumbani na baba yake wakati alipokuwa hospitali ya rufaa Mbeya.

Watuhumiwa  wa kesi hiyo ni pamoja na Cosmas Yoram Songoloka (baba wa mtoto) Andius George Songoloka, Unela Shinji Jiloya Seme (anayedaiwa kukiri polisi kwamba ndiye aliyekata kiganja na ndiye aliyewaongoza polisi hadi kumkamata ‘tajiri’ Kalinga), na Mihambo Kanyenga Kamata maarufu kama Bichi (ambaye ni mganga wa jadi) na Sajenti Kalinga (Tajiri aliyetaka kununua kiganja hicho kwa Milioni 100) ambao walikambatwa tangu April mwaka 2015.

Katika kusoma hukumu hiyo Jaji John Mgeta alimuacha huru baba wa mtoto baada ya upande wa mashtaka kuwa ushahidi hafifu wa kumtia hatiani na hivyo kushindwa kuthibitisha bila ya shaka uhusika wake ushahidi kushindwa kumtia hatiani baba huyo
Mnunuzi wa kiungo hicho Sajenti Kalinga alipewa kifungo cha miaka 8 jela kwa kukutwa na kiganja na kukiri kosa tangu mwanzo na pia kutoa ushirikiano kwa vyombo vy a usalama.

Kwa upande wa Andius George Songoloka, alipatikana na hatia ya makosa matatu, kula njama ya kuua – alifungwa miaka 10, jaribio la kuua mtoto mlemavu wa Ngozi – alifungwa miaka 15 na kumsababishia ulemavu wa kudumu- alifungwa miaka 18.

Unela Shinji Jiloya na Miambo Kanyenga Kamata walikutwa na makosa mawili jaribio la kuua mtoto mlemavu wa Ngozi – walifungwa miaka 15 na kumsababishia ulemavu wa kudumu- walifungwa miaka 18. Hatimae kutumikia kifungo cha miaka 18 jela kwa kila mmoja.
Alisema kosa la kula njama ya kuua, adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 215 ya kanuni ya adhabu sura 16, huku kosa la kufanya jaribio la kutaka kuua adhabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 211 ya kanuni ya adhabu sura 16 na kosa la kusababisha ulemavu wa kudumu adahabu yake ni kifungo cha maisha jela kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 222 ya Kanuni ya adhabu sura 16.

Utetezi

Katika kesi zote viungo hivyo vilichochukuliwa kutoka kwa washtakiwa hao kilipelekwa kuchunguzwa vinasaba (DNA) kwa lengo la kuthibitisha iwapo vilikuwa vya waathirika.
Mtoto Baraka Cosmas (Kulia) akiwa na Mwenziwe Mwigulu Matonange (Kushoto)

Waliokuwa wakitetewa na mawakili wanne ambao ni Bartazar Chambi, Charles Kasuku, Peter Kamyalile na Mathias Budodi   
                           
Awali, Wakili wa Serikali Fadhili Mwandoloma aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotenda makosa kama hayo.

Nao, mawakili wa upande wa utetezi waliiomba mahakama kupunguza adhabu kwa wateja wao kwa kuwa tayari wamekaa mahabusu kwa zaidi ya miaka minne kitu ambacho ni funzo tosha kwao hivyo hawawezi kurudia kutenda tena makosa hayo.
Baraka Cosmas na Wenziwe walipopelekwa New York Marekani kwaajili ya kupatiwa viungo vya bandia.